Habari

Mradi wa TVET kuwanufaisha Vijana nchini

Mradi wa TVET kuwanufaisha Vijana nchini

Mradi wa TVET ni mradi wa kuongeza ujuzi kwa Vijana ili waweze kujiajiri na kupata nafasi za kuajirika Duniani ambao unatumika kupitia vyuo vya ufundi vyenye matawi ya RAAWU pekee

 

Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) ni mmoja wa waratibu wa mradi huo wa TVET nchini, ambapo Katika Warsha iliyofanyika nchini Denmark, (RAAWU) iliwakilishwa na Mratibu wa jinsia na Kaimu Katibu wa Elimu Bi. Mariam Mgalula.

Mradi huo umeanza Katika mikoa miwili Dar es salaam na Morogoro Katika vyuo vya  VETA Dar es salaam, VETA Kihonda, VETA Mikumi na Chuo Cha Don Bosco Osterbay jijini Dar es salaam.

Mradi huo unafadhiliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Denmark (DTDA) na Chama Cha waajiri Nchini Denmark (DI) huku Nchini Tanzania wakishirikisha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)  na Chama Cha waajiri (ATE).

TUCTA Katika mradi huu imekuwa sambamba na vyama vyake shiriki viwili ambavyo ni RAAWU na TUICO  kutokana na zoezi Zima la kuwashirikisha walimu na wanafunzi kutoka Katika Vyuo hivyo vya ufundi sambamba na Viwanda ambapo mafunzo ya vitendo yanafanyika huko.

Mradi wa TVET umelenga kuboresha mahusiano Bora kwa TUCTA na ATE, kuboresha ufanisi kwa Vyuo vya VETA na Donbosco, unaongeza ujuzi kwa Vijana kwani Vijana 900 Nchini Tanzania, wanawake na wanaume wanategemewa kupata Elimu hii Kwa ufadhili wa mradi huo.

KARIBU RAAWU

Makao Makuu

    • Bibi Titi/Sophia Kawawa Street
    • P. O. Box 22532 Dar-es-Salaam
    • Tel: +255-22-2123762
    • Fax: +255-22-2123762
    • Email: info@raawu.or.tz
    • Website: www.raawu.or.tz