Kuhusu Sisi

Kuhusu RAAWU

Maana Ya Chama Cha Wafanyakazi

Ni muungano wa Wafanyakazi wa sehemu au sekta husika ya kazi, unaotokana na ridhaa yao wenyewe kwa lengo la kulinda, kutetea haki na maslahi yao. Muungano huu hatimaye hutambuliwa rasmi na mamlaka ya nchi baada ya kusajiriwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo. Kwa Tanzania Sheria namba 6 na 7 za mwaka 2004 ndizo zinayosimamia vyama vya wafanyakazi.

MAANA YA RAAWU RAAWU ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza “Researchers Academicians and Allied Workers Union”. Neno hili limetafsiriwa Kiswahili kukidhi matakwa ya wanachama wetu; yaani Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Stadi, Ushauri, Habari na Utafiti.

KUUNDWA KWA RAAWU

Kuundwa kwa RAAWU kulitokana na mabadiliko katika historia ya Vyama vya Wafanyakazi nchini, kutoka katika mfumo wa chama kimoja cha wafanyakazi NUTA /JUWATA (1964-1991) na kuingia kwa mfumo unaoruhusu Wafanyakazi kujiundia Vyama vyao kulingana na sehemu au sekta wanazotoka. RAAWU ni miongoni mwa vyama huru kumi na moja (11) viliundwa chini ya Sheria ya OTTU namba 20 ya mwaka 1991. Mkutano Mkuu wa kwanza wa RAAWU uliofanyika mwezi Novemba 1994, ndio uliohitimisha uundaji wa chama hicho baada ya kupitisha katiba na kuchagua viongozi wa kitaifa. RAAWU vilevile ni chama huru kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya wafanyakazi No. 10, 1998. Mwaka 2000 RAAWU iliitisha Mkutano Mkuu wa Tatu ambao ulifanya marekebisho ya Katiba na Kuchagua viongozi wapya wa kitaifa. Aidha mkutano huo ulipitisha maazimio kadhaa yanayolenga katika kuboresha maisha ya wanachama na jamii kwa ujumla.

DIRA YA RAAWU (VISION)

Kuwepo kwa jamii ambamo watu wana haki ya kufanya kazi, Vyama imara vya Wafanyakazi vinavyoendeshwa kidemokrasia na kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa mahitaji yao ya kijamii na kiuchumi.

LENGO LA RAAWU (MISSION)

Lengo la RAAWU ni kuboresha mazingira ya kazi kwa wanachama wake, kushirikisha wanachama katika kufikiwa kwa maamuzi ya chama, kushinikiza juu ya kuwepo kwa sera zitakazoinua na kukuza nafasi za ajira na kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanakuwa na maisha bora wakiwa kazini na baada ya kustaafu. RAAWU imejishirikisha na:- • Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA). • Shirikisho la kimataifa linalohudumia wafanyakazi wa sekta za huduma kwa Umma “Public Services Interational” (PSI).

RAAWU

Sauti Ya Wafanyakazi

MADHUMUNI YA RAAWU

(a) Kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya wanachama katika maisha yao wakiwa kazini na baada ya kustaafu.

(b) Kushirikiana na kujadiliana na waajiri katika kudumisha amani mahala pa kazi.

(c) Kujadiliana na kuondoa tofauti zinazojitokeza baina ya mwajiri na mwanachama, au mwanachama mmoja na mwingine kwa njia ya makubaliano ya amani kadri inavyowezekana.

(d) Kushiriki katika kusaidia utekelezaji wa mikataba ya hali bora za kazi, tuzo, kanuni za nidhamu na kanuni zozote zile ambazo zinatumika nchini.

(e) Kushirikiana na kubadilishana ujuzi na vyama vingine vya wafanyakazi nchini pamoja na vile vya Kimataifa.

(f) Kuwasiliana na Serikali kuhusu utungaji wa sheria sahihi za kazi na kuandaa sera nzuriza kuendeleza maisha ya jamii.

(g) Kulinda maslahi ya wanachama kwa kuhimiza Serikali kuepukana na uandaaji wa sera ambazo ni hatari kwao.

Mradi wa TVET

RAAWU katika Mradi wa TVET

Mradi wa TVET ni mradi wa kuongeza ujuzi kwa Vijana ili waweze kujiajiri na kupata nafasi za kuajirika Duniani ambao unatumika kupitia vyuo vya ufundi vyenye matawi ya RAAWU pekee

Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) ni mmoja wa waratibu wa mradi huo wa TVET nchini, ambapo Katika Warsha iliyofanyika nchini Denmark, (RAAWU) iliwakilishwa na Mratibu wa jinsia na Kaimu Katibu wa Elimu Bi. Mariam Mgalula.

Mradi huo umeanza Katika mikoa miwili Dar es salaam na Morogoro Katika vyuo vya  VETA Dar es salaam, VETA Kihonda, VETA Mikumi na Chuo Cha Don Bosco Osterbay jijini Dar es salaam.

Mradi huo unafadhiliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Denmark (DTDA) na Chama Cha waajiri Nchini Denmark (DI) huku Nchini Tanzania wakishirikisha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)  na Chama Cha waajiri (ATE).

KARIBU RAAWU

Makao Makuu

    • Bibi Titi/Sophia Kawawa Street
    • P. O. Box 22532 Dar-es-Salaam
    • Tel: +255-22-2123762
    • Fax: +255-22-2123762
    • Email: info@raawu.or.tz
    • Website: www.raawu.or.tz