Viongozi wa RAAWU Taifa

Viongozi wa RAAWU Taifa katika picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya RAAWU Tawi la TIRDO jijini Dar es salaam

Viongozi wa RAAWU Taifa

Viongozi wa RAAWU taifa wakiwa Pamoja na Menejimenti ya TIRDO

Ziarani Dar es salaam

Viongozi wa RAAWU Taifia wakiwa Ziarani Dar es salaam kutembelea wanachama 

Mradi wa TVET ni mradi wa kuongeza ujuzi kwa Vijana ili waweze kujiajiri na kupata nafasi za kuajirika Duniani ambao unatumika kupitia vyuo vya ufundi vyenye matawi ya RAAWU pekee

Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) ni mmoja wa waratibu wa mradi huo wa TVET nchini, ambapo Katika Warsha iliyofanyika nchini Denmark, (RAAWU) iliwakilishwa na Mratibu wa jinsia na Kaimu Katibu wa Elimu Bi. Mariam Mgalula.

Mradi huo umeanza Katika mikoa miwili Dar es salaam na Morogoro Katika vyuo vya  VETA Dar es salaam, VETA Kihonda, VETA Mikumi na Chuo Cha Don Bosco Osterbay jijini Dar es salaam.

Mradi huo unafadhiliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Denmark (DTDA) na Chama Cha waajiri Nchini Denmark (DI) huku Nchini Tanzania wakishirikisha Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)  na Chama Cha waajiri (ATE).

RESEARCHERS, ACADEMICIAN AND ALIED WORKERS UNION (RAAWU)

Ni muungano wa Wafanyakazi wa sehemu au sekta husika ya kazi, unaotokana na ridhaa yao wenyewe kwa lengo la kulinda, kutetea haki na maslahi yao. Muungano huu hatimaye hutambuliwa rasmi na mamlaka ya nchi baada ya kusajiriwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo. Kwa Tanzania Sheria namba 6 na 7 za mwaka 2004 ndizo zinayosimamia vyama vya wafanyakazi.